KUWA NA MTAZAMO CHANYA KATIKA MAISHA YAKO YA BAADAE (TAKE CONTROL OF YOUR FUTURE).
Ndugu tupo tupo kwenye mwendelezo wa kujifunza ni namna gani
tunaweza kupiga hatua katika maisha yetu. Leo napenda tuangalie kwanini unahitaji kuwa na kazi yako?
Kuwa
na mtazamo chanya katika maisha yako ya baadae (Take control of your future.)
hebu tuangalie kwa kina kwanini unahitaji kuwa na kazi yako
1.UTARATIBU UMEBADILIKA (THE RULES
HAVE CHANGED.)
Tunaishi wakati wa shida sana .
miaka michache iliyopita mfumo wa maisha ulikuwa tofauti kabisa na sasa hivi.
Fikiria maisha ya karne ya 20 iliyopita ujaribu kulinganisha na leo. Asilimia
kubwa ya watu wa leo wanasema uchumi umekuwa kati ya majanga makubwa katika
maisha ya watu. Watu wengi wamekuwa wakiishi katika upande wa makali ya visu
wengi wao wakiishi wakiwa hawana uhakika wa kesho watafanya nini?. Ni kweli
natambua haya pengine unayajua lakini
unatambuaje kuhusu ni namna gani mtu anaweza kusimama hadi kufikia sehemu anayoitaka.Mtazamo
chanya pekee ni suluhisho pekee katika kufikia ndoto zako.
2. NIMEKWAMBIA HIVYO (I TOLD YOU SO).
Umeshawahi
kujiuliza na kutafakari ni kazi gani ambayo inaweza kuwa salama kwako? Sitaki
kukatisha tamaa lakini Ukweli wa uhalisia ni kwamba hakuna kazi ambayo ipo
salama siku zote. Lakini je unatafakari vipi kuhusu mtazamo wako katika maisha
yako ya baadae. Unaweza kutupia lawama katika ngazi za juu n.k. lakini wewe
kama wewe unasimamaje katika kutetea maendeleo yako.
3.HII NI KARNE MPYA (IT’S A NEW CENTRUY ).
Wakati
nilipokuwa mtoto, wazazi wangu walinisihi njia sahihi ya kupata mafanikio
ambayo ni ya uhakika ambayo nina imani hata wewe ulisihiwa ni kwamba:- Mwanangu
nenda shule, kasome kwa bidii upate maksi nzuri ili uje upate kazi nzuri na
ulipwe pesa kubwa na ili upate kazi kwa urahisi.
Lakini ndugu, napenda nikwambie hii ni karne mpya na siyo tu karne mpya bali hadi mawazo ni mapya.
Ndugu kazi haiwezi kukuweka huru wala
serikali haiwezi kukuweka huru bali mawazo yako ndio chombo pekee
kitakachokuweka huru katika maisha yako yote..
4. MSTARI WA KIJANI AU MWEKUNDU.
Nimeita ni mstariwa kijani au mwekundu kwa sababu
nikiangalia idadi ya watu waliopo ajirani kwenye mstari wa umaskini yazidi
kupanda na idadi kubwa ya watu wanaofanya kazi zaidi ya umri wa miaka 60
yaongezeka. Na ninakuja napoteza maana halisi ya neno kustaafu maana sasa wazee
wanapostaafu inakuwa kama ndio umefika muda wao wa kufanya kazi hakika
nashindwa kuona mbele maana ni kiza tu lakini hapo hapo natambua ni kwa nini
nahitaji kuwa na kazi yangu mapema .Tukiwa tunazidi kujifunza hebu naomba
utafakari hayo na ninakuomba usikose hata makala moja zijazo karibu tena katika
mwendelezo wa makala hii.

0 comments: