Ndoto
imekuwa ni kitendawili ambacho kimekuwa kikikosa jibu la moja kwa moja baina ya
watu na kufanya wengi wao wakate tamaa katika safari yao ya kutimiza ndoto zao.
Leo napenda kuzungumzia mambo yafuatayo yatakayokusaidia kupiga hatua katika
mafanikio yako:-
1.
KUWA IMARA.
Mafanikio yetu yanategemea sana uimara wetu hasa katika upande wa afya
zetu,ndugu kama itazolota na kulegea kweli upande wa kufikia malengo yako
itakuwa ni kitendawili. Maana afya zetu zinapokuwa imara hapo tunaweza
kukumbuka tufanye nini ili kufikia mahala Fulani tunapotaka kufika.
2.
FURAHIA MAISHA YAKO.
Ni kosa la jinai sana inapofikia hatua tunaanza kulaani maisha tuliyonayo
, wengi tumekuwa tukilaani sana maisha tuliyonayo kwa sababu ya ugumu wake, changamoto
zake n.k. lakini hatukumbuki kupitia hayo maisha tuliyonayo ni fursa pekee
ambayo tunaweza kufanya vitu vikubwa ambavyo mwisho wa siku tutafurahia maisha yetu.
Ndugu tunapofurahia maisha yetu inatupa chachu na hamasa zaidi katika kufight
ndani ya maisha yetu na ndo kitu pekee kitakachomfanya mtu atomize ndoto zake
haraka akiwa atafurahia nafasi aliyonayo na kuweza kufanya kazi kwa bidii zote.
3.
FANYA UTALII.
Neno utalii linakuja linatafasiriwa tofauti linapokuja kwenye mindset za
watu kuwa hadi usafiri nje ya nchi ndo uwe umefanya utalii. Utalii upo wa aina
nyingi ukiwa ni wa nje au wa ndani na ya
nchi. Ndugu unapokuwa unafanya utalii ni nafasi kubwa ya kuweza kujifunza mambo
mengi yakiwemo biashara, kilimo, mazingira ya kuishi, uwekezaji n.k. maana
unapokuwa unaishi mazingira yaleyale kila kukicha huingizi kitu chochote kichwani,
yaani hujaona kitu kipya kwa muda mrefu kuna percentage kubwa sana ya akili
kudumaa na kuona kumbe maisha ni hayahaya kwahiyo unapofanya utalii wa
mazingira tofauti tofauti unafanya akili yako ifunguke kwa mambo mengi.
4.
TUNZA PESA.
Kati ya vitu ambavyo imekuwa ni mtihani mkubwa mzito ni namna gani ya
kutunza pesa? Pesa imetawala kabisa fikira za watu na kushindwa ni namna gani
ya kuikabili wanapoipata. Si rahisi sana kutambuia kama pesa inakutawala au laa
lakini unapoweza kutunza pesa na kuweza kuifanyia vitu vya msingi
ulivyoipangilia kabla hujaipata itakuwa ni rahisi sana kutimiza ndoto zako.
5.
SAIDIA WENGINE.
Kusaidia ni jambo jema ambalo linatakiwa lifanywe kwa kila mmoja wetu. Ndugu
tunapokuwa na moyo wa kutoa na kusaidia wengine tunajijengea tabia ya kupokea
na sisi na moyo wa utafutaji zaidi maana unapokuwa unatoa unajiandaa kupokea
pia.
6.
TAFUTA KAZI MPYA.
Kazi unayofanya isiwe ni kikwazo cha kufikia ndoto zako wengi tumekuwa
tukishindwa kuchukua maamuzi yaliyo sahihi hata kama mzigo umetuelemea katika kazi zetu kwa kuhofia kushindwa kazi nyingine.
Pale panapohitaji kuchukuliwa maamuzi yachukuliwe tu maana huwezi jua kilicho
mbele yako kabla hujafika huko.