Tuesday, September 25, 2018

KIJANA NA HAMASA: CHANGAMOTO YAKO NI IPI?


Ni siku nyingine tena ,kwa imani wewe ni mzima wa afya tele na ni tumaini langu hujambo kabisa.
Matatizo, Shida, Changamoto n.k Wengi wetu imekuwa ni sehemu ya maisha yetu, lakini je umewahi kujiuliza Changamoto yako ni ipi?
Changamoto zipo za kila aina zikiwemo changamoto za kiafya, Elimu, Uchumi kuyumba, Mila, Utamaduni n.k. Kwa leo napenda tutafakari juu ya changamoto ambayo imekuwa kilio kwa wengi wetu ambayo ni changamoto ya uchumi.
Ndugu katika makala zangu nimekuwa nikihusisha sana maswali siyo kwamba nataka nikusumbue ila nataka ujaribu kuumiza kichwa ,uwe mtu waku-reason yaani ushirikishe akili kutatua changamoto mbalimbali katika maisha yako. Changamoto ya Uchumi imekuwa ni kwa kila mtu si kwa maskini au matajiri lakini je umejaribu kufikiria ni sababu gani zinazosababisha iwe hivyo.
Katika siku ya leo napenda tutafakari sababu zifuatazo ambazo kwa upande wangu nahisi zimekuwa ni tatizo na chanzo kwa watu wengi kuyumba kwa uchumi.
Kwanza changamoto kubwa katika upande wa kujiinua kiuchumi ni Kutokujiamini kuthubutu (Wasiwasi) na Uzembe. Kitabu cha Retire young retire rich by Robert T. Kiyosaki aliandika“The biggest challenge you have is to challenge your own self-doubts and your laziness”Ndugu hebu jaribu kujitathimini upo kwenye dimbwi hili? Je ni fursa ngapi zimekupita ukiogopa kwamba wewe hauwezi na haustahili kufanya hivyo? Au ni kazi ngapi ambazo umekuwa mzembe wakufanya kwasababu za kusingizia mbalimbali. Robert T. Kiyosaki aliendelea kuandika “It is your self-doubts and your laziness that define and limit who you are” Kwa maana ya kwamba ni wasiwasi wako na uzembe wako unaokutambulisha na kukuonyesha kikomo chako jinsi gani ulivyo. Halafu akaendelea kusema “There is no one in your way except you and your doubts and If you will take on your self doubts and your laziness, you will find the door to your freedom”kwa maana ya kwamba “Hakuna njia yeyote tofauti na wewe na wasiwasi wako na kama utapata ufumbuzi wa wasiwasi wako na uzembe wako hakika utapata mlango wa uhuru wako.”
Note; Siku zote maamuzi sahihi ni yale anayoyachukua mtu bila kushirikishwa, kuna tofauti kubwa sana kati ya maamuzi na ushauri maana ushauri unaweza kuukubali au kuukataa lakini maamuzi yako ni msingi wa maisha yako.

Changamoto zipo nyingi sana na mtu sahihi wa kutatua changamoto yako ni wewe mwenyewe kikubwa ni kuamini unachokifanya kuwa ni sahihi. Naomba tukutane kwa makala nyingine tena katika makala zijazo katika mwendelezo wa makala zinazohusu kupata pesa na kuendelea kuwa na pesa na kutakia uwe na siku njema.

0 comments: