Kufeli
katika mipango au mikakati uliyojiwekea ni kitu ambacho kinatokea kwa kila mtu.
Na ni wakati ambao mtu anakuwa njia panda katika kufanya maamuzi ama kuendelea
au kuacha.
Wakati
unapopitia hatua hii katika mipango yako huu sio wakati wa kuruhusu na
kukufanya wewe uweze kukata tamaa katika safari yako badala yake unatakiwa
upanue ufahamu wako ujue ni namna gani ya kuendelea na kukufanya ufike pale
ulipotaka kufika.
Ndugu
napenda kukuambia kitu cha msingi sana ambacho unatakiwa kukifanya endapo
utaanza kuona dalili za kufeli katika mipango yako, kwanza unatakiwa ujue
kwamba hutakiwi kujiona kama wewe ni mkamilifu kwa kitu ambacho unakifanya (do not need to be perfect or
perfectly extraordinary just be better version of you)
Mara nyingi
tumekuwa tukiangalia hasa mabadiliko ya vitu tunavyovifanya tukisahau kuangalia
mipangilio yetu ikoje na inaendeleaje? Kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuona
mabadiliko hakumanishi kama mipango yako imekufa au laa , hapo kinachotakiwa na
kusubiriwa ni wewe kujua unatakiwa upangilie kwa namna gani ili uweze kuona
mabadiliko unayoyataka. Mwandishi mmoja aliandika “When you have a day
when you fall down on the diet, instead of telling yourself that you are weak
or bad, tell yourself that you had a bad day and that tommorrow’s a new day to
start is over.”
Ni muhimu
sana kuwa mstahimilivu , kuwa na upeo wa kutambua kitu mapema itakusaidia sana
kusonga mbele katika safari yako halafu tambua ni rahisi sana kukata tamaa
kuliko kujipa moyo hivyo badala ya kuruhusu mawazo hasi yanayokujia kwenye
ufahamu wako ni muda sasa wa kuwa na mawazo chanya na kuondoa yote mawazo
mawazo ambayo yatakupelekea kukata tamaa katika kufikia ndoto zako.



0 comments: