Tupo
kwenye dunia (Ulimwengu) ambao kila mtu anapambana ili afanikiwe katika maisha
yake. Sizani na sijawahi sikia mtu anayehitaji maisha ya shida lakini pamoja na
hayo yote tatizo linakuja kwenye kufikia hayo mafanikio
Katika siku ya leo napenda tuangalie vitu vitatu ambavyo
vinaweza kuwa chachu ya maendeleo na hatimaye kufikia ndoto.
Kwanza kuwa na malengo (Write down
the goal). Mafanikio yeyote yanakuja pale penye malengo japo kwa
mwanadamu wa sasa anakuambia hakuna asiye na malengo lakini je unafikia hayo
malengo?. Malengo ni kitu pekee kinachomfanya mtu afikie mahali anapopahitaji
mfano mzuri ni kwamba hauwezi kuwa na safari ambayo utasafiri usijue mwisho au
kituo cha safari yako ni wapi?. Maana hauwezi kutoka Dar es salamu ukafika
Mwanza kama hujui unaelekea Mwanza na kwahiyo hauwezi ukafikia malengo yako
kama huna malengo.
Pili Tengeneza Mipango (Create plan)
ndugu yangu malengo bila mipango ni kazi bure,maana hauwezi ukafikia malengo
yako bila mipango ya kuweza kukufanikishia.hebu chukulia mfano wetu wa kwanza.
Safari yetu ni kutoka Dar es salam kuelekea Mwanza (kwa maana Dar es salaam
ndipo ulipo na unaelekea mwanza sehemu unayoenda kushuka) Swali linakuja sasa
Unatokaje Dar es salaam kufika Mwanza? Halafu unapita wapi na wapi hadi ufike
Mwanza? Ukishapata majibu ya maswali hayo naamini itakuwa sawasawa na namna
gani unaweza kupanga mipango yako na kufikia malengo yako.
Tatu na Mwisho Amini Mawazo yako (Believe
and Focus on your idea) Najua kuna vitu ambavyo unafikiria na unawaza
kuvifanya lakini hujiamini na unaona ukifanya unaweza kufeli na kuweza kuaibika
lakini nikwambie mawazo yako ndio kila kitu katika kutimiza ndoto zako hebu
amka na ufanye kile unachowaza uone ni jinsi gani ulikuwa umechelewa kutimiza
ndoto zako. Ndugu yangu silaha kubwa ya mafanikio ni imani yako katika kazi
yako.
Ndugu yangu, kwa leo naamini umenielewa na kupitia mifano
hiyo itakuwa ni chachu kwa mafanikio yako naomba tukutane tena kwa makala
zijazo kwa mawasiliano na ushauri zaidi