Thursday, May 17, 2018

KIJANA NA HAMASA: NAMNA YA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.

Tupo kwenye dunia (Ulimwengu) ambao kila mtu anapambana ili afanikiwe katika maisha yake. Sizani na sijawahi sikia mtu anayehitaji maisha ya shida lakini pamoja na hayo yote tatizo linakuja kwenye kufikia hayo mafanikio
Katika siku ya leo napenda tuangalie vitu vitatu ambavyo vinaweza kuwa chachu ya maendeleo na hatimaye kufikia ndoto.
Kwanza kuwa na malengo (Write down the goal). Mafanikio yeyote yanakuja pale penye malengo japo kwa mwanadamu wa sasa anakuambia hakuna asiye na malengo lakini je unafikia hayo malengo?. Malengo ni kitu pekee kinachomfanya mtu afikie mahali anapopahitaji mfano mzuri ni kwamba hauwezi kuwa na safari ambayo utasafiri usijue mwisho au kituo cha safari yako ni wapi?. Maana hauwezi kutoka Dar es salamu ukafika Mwanza kama hujui unaelekea Mwanza na kwahiyo hauwezi ukafikia malengo yako kama huna malengo.
Pili Tengeneza Mipango (Create plan) ndugu yangu malengo bila mipango ni kazi bure,maana hauwezi ukafikia malengo yako bila mipango ya kuweza kukufanikishia.hebu chukulia mfano wetu wa kwanza. Safari yetu ni kutoka Dar es salam kuelekea Mwanza (kwa maana Dar es salaam ndipo ulipo na unaelekea mwanza sehemu unayoenda kushuka) Swali linakuja sasa Unatokaje Dar es salaam kufika Mwanza? Halafu unapita wapi na wapi hadi ufike Mwanza? Ukishapata majibu ya maswali hayo naamini itakuwa sawasawa na namna gani unaweza kupanga mipango yako na  kufikia malengo yako.
Tatu na Mwisho Amini Mawazo yako (Believe and Focus on your idea) Najua kuna vitu ambavyo unafikiria na unawaza kuvifanya lakini hujiamini na unaona ukifanya unaweza kufeli na kuweza kuaibika lakini nikwambie mawazo yako ndio kila kitu katika kutimiza ndoto zako hebu amka na ufanye kile unachowaza uone ni jinsi gani ulikuwa umechelewa kutimiza ndoto zako. Ndugu yangu silaha kubwa ya mafanikio ni imani yako katika kazi yako.
Ndugu yangu, kwa leo naamini umenielewa na kupitia mifano hiyo itakuwa ni chachu kwa mafanikio yako naomba tukutane tena kwa makala zijazo kwa mawasiliano na ushauri zaidi


                                                                    

1 comment: