Ni siku nyingine tena tukiendelea na mfululizo wa makala
hizi kwa undani zaidi siri ya kupata pesa (Utajiri) na kuendelea kuwa na pesa
(Utajiri).
Watu wengi wamekuwa wakizunguka huku na huko wakitafuta hasa
nini siri ya utajiri na wengine hadi kukimbilia imani potofu ili mradi tu
wapate mali (Utajiri). Ni njia gani rahisi ambayo inaweza kuleta mafanikio kwa
uharaka hili limekuwa ni swali ambalo linatawala vichwa vya wengi.
Na kitu kinachoponza zaidi ni pale mtu anapohitaji mafanikio
kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Ndugu
leo napenda nikupe siri moja tu ya mafanikio ambayo inaweza kuwa njia ya pekee
ya kukuvusha daraja katika maisha yako.
Mafanikio hayatafutwi kwa dawa au zile imani potofu
wanavyodai wengi. Mafanikio yanakuja pale mtu unapotambua anataka nini katika
maisha yake. Maana yake kwanza anatakiwa atambue kwanini anataka utajiri au
mafanikio? Halafu baada ya hapo akishapata sababu za kwanini anataka kuwa
tajiri atafute sasa ni njia gani au namna jinsi afanye ili aweze kujikwamua
sehemu alipo siyo kutafuta njia rahisi tu na ya haraka.
Watu wengi wamekuwa wakihoji na kuuliza kwa watu
waliofanikiwa katika maisha yao kwamba ni njia gani wametumia hadi kufanikiwa?
Jibu la moja kwa moja hapo ni kwamba huwezi ukajua ni njia gani zinazomfanya
mtu afanikiwe kama hujajua kwanini unataka ufanikiwe katika maisha yako?.
Maana mfano mzuri ni kwamba wengi husingizia tatizo ni mtaji lakini ni wangapi
ambao wanakuwa na pesa za kuanzisha kitu chochote lakini anakaa muda mfupi tu
anakuwa hana kila kitu kwahiyo ndugu kama hujajua kwanini unataka kuwa na
mafanikio huwezi ukajua ni njia gani za kukufanya uwe na mafanikio.
Katika siku ya leo naomba uchukue tathimini dogo na ya haraka
katika maisha yako Ni kweli katika maisha yako
hujawahi kupata pesa ambayo kwa leo unafikiria ingekuwa mtaji kwako? Au Ni
fursa ngapi umezipata hapo nyuma ambazo unafikiria ungekuwa nazo leo ungekuwa
umejikwamua na maisha yako? Ndugu ukipata majibu ya maswali hayo naamini
utakuwa umenielewa na kuelewa hasa nini siri kubwa ya mafanikio?
Sipo hapa kukukatisha tama maana unajua ni wapi ulipita
lakini cha msingi hebu tafakari sasa kwa makini halafu ufanye yafuatayo;
1.
Acha kuendelea kuongea tu (Stop talking) najua una mipango mingi sana lakini cha
kukushauri hebu acha kuishia kuwaza na kuongea tu na kuendelea kupanga kila siku.
2.
Toa ndoto zisizo na kikomo (Stop dreaming) hizo ndoto ulizonazo haziwezi kutimia
kwa kuwa nazo bila utekelezaji.
3.
Chukua hatua madhubuti ( Start Commiting) huu ni wakati wako kuanza kutekeleza kile
unachokihitaji katika maisha yako acha woga mawazo yako ni sahihi hebu jaribu
kutembea na hisia zako ili uweze kufanikiwa katika maisha yako.
Ndugu nashukuru sana kwa siku yako kuweza kufuatilia huku nikiamini umenielewa na hili litakuwa ni
chachu kubwa ya mafanikio yako ahsante sana kwa muda wako kwa siku ya leo
naomba tukutane tena kwa makala zijazo ili tuendelee kujifunza zaidi kuhusu
maisha yetu ni ukutakie uwe na siku njema

hakika mafanikio yanakuja pale mtu anapoamua kuthubutu
ReplyDelete