Friday, June 8, 2018

KIJANA NA HAMASA: PANGA KUSTAAFU.

Nini maana ya kustaafu?
Kustaafu ni kuacha kazi kwa mujibu wa sheria , ama baada ya mkataba kuisha au kwa kuomba kutokana na sababu mbalimbali kama za kiafya n.k
Kwa nini Ustaafu?
Kwa haraka haraka mtu anaweza kujiuliza. Nini maana yangu ya kuandika kichwa cha Kupanga kustaafu kama ninajua umeajiriwa au haujaajiriwa? Wengi wetu tunajua neno kustaafu linatumika tu hasa kwa Watumishi wa Umma au Makampuni. Hapana kustaafu anaweza kustaafu mtu yeyote kwenye kazi yake kutokana na sababu mbalimbali. Na mimi siku ya leo napenda kukushauri upange kustaafu hebu twende moja kwa moja ujue ni kwanini?
Nianze kwa kukuambia, Mwandishi wa kitabu cha Retire young retire rich aliandika “Most people do not think about retiring  until its too late.”    Kabla sijaendelea naomba nikukumbushe makala ya nyuma nilitolea mfano wa safari ya kwamba huwezi ukasafiri ukafikan hujui point yako ya mwisho (destination point.) Wengi wetu tunajisahau sana kuhusu hili neno kustaafu tukitarajia hadi tufikie uzeeni.
Kustaafu hakumanishi tu hadi uwe mzee au uajiriwe serikalini, Je hufikirii kwa kazi hiyo uliyo nayo itafika muda ushindwe kufanya sawasawa na leo? Au hujui kama fursa za leo si za kesho? Panga kustaafu, Si lazima ufikie miaka 60 au zaidi ndio ufikirie kustaafu hebu angalia maisha yako ya kesho yatakuwaje?
Ninapozungumzia kupanga kustaafu simanishi uache kazi najaribu kukumbusha uwe na mipango ya kufanya kazi ambayo itakufanya ustaafu mapema kwa maana ya kuwa na kazi ambayo itakuwa inakufanyia kazi siyo kuendelea kufanya kazi hadi uzeeni.
Safari ya mafanikio ni kitendawili ambacho kimekuwa hakina jibu la moja kwa moja na inapotokea unasafiri safari ambayo hujui utakuwa na mapumziko ni sawa na kuwa mtumwa bila kujijua. Kuna vitu vingi unavyotakiwa kufanya lakini  hebu jaribu kuweka muda wa kufikiria ni lini utapumzika katika safari yako hiyo?
Tupo vijana wengi tunaopata pesa na kuwa na matumizi ambayo hayafai bila kufikiria kwamba nafasi tuliyo nayo leo hatujui kama itaendelea kuwepo hadi kesho hali ambayo itakuja itugharimu katika uzee wetu na kubaki kulaani bila sababu. Ndugu inawezekana kabisa kupata pesa na kuendelea kuwa na pesa katika maisha yetu yote kama tutakuwa na mawazo chanya katika maisha yetu ya kila siku
Kwa leo naomba tuishie hapa naomba tukutane tena kwa makala zijazo kwa ajili ya kujifunza zaidi ni mimi muhamasishaji wako