Ndugu, Mpendwa ni tumaini langu wewe ni mzima wa afya
tele. Itakuwa ni jambo njema ukichukua muda hata wa dakika moja uweze
kumshukuru Mungu kwa hii nafasi uliyoipata siku ya leo. Maana kuna ambao
walitamani kuiona siku hii lakini haikuwezekana.
Katika siku ya leo napenda nifungue ukurasa mpya ambao
umekuwa ni changamoto kwa watu wengi sana wakiumiza vichwa ni namna gani ya
kupata pesa(Utajiri) na kuendelea kuwa nayo siku zote.
Hebu tuweze kuangalia kwa undani ni namna gani NGUVU YA MAWAZO
YAKO inaweza kukufanya upate
pesa, halafu uendelee kukaa na pesa siku zote. Imefikia hatua hadi watu
wanafanyiwa tunguli kwa sababu ya kulinda pesa zao lakini napenda nikuibie siri
nzito sana leo.
Katika vitu vyenye nguvu na ambavyo vinafanya mtu
afanikiwe ni uwezo wa akili yako (Power of your Mind), Tatizo linakuja pale
Nguvu na Uwezo wa akili yako inapofanya kazi katika upande sahihi au usio
sahihi. Mwandishi mmoja wa Kitabu aliandika (“One big
difference between the rich and the poor is that poor people says “I can’t
afford it;” more often than rich”) “Tofauti
kubwa kati ya mtu tajiri na Mtu maskini ni Kwamba Maskini husema “Siwezi
kufanya hiki” Tofauti na watu matajiri halafu
akaendelea kusema (“Poor people use poor words and poor words create poor people means
Your words do become flesh”) “Watu maskini hutumia
maneno ya kimaskini na maneno ya kimaskini hutengeneza watu maskini” na maneno
yako waswahili wanasema Maneno huumba.
Katika ukurasa huu, ndugu naomba ujifunze tofauti ya
maneno ya tajiri na maneno ya maskini , maneno yenye kasi kubwa na maneno yenye
kasi ndogo na katika hili utatambua ni namna gani unaweza kubadilisha maisha
yako kwa kutumia maneno yako na jinsi gani unavyofikiria na kama utaweza
kubadili maneno yako na mawazo yako kama matajiri, ukawa na mawazo chanya naamini ukipata pesa , utaendelea kuwa na
pesa kwa urahisi sana
Ahsante
sana kwa siku ya leo naomba tukutane kwenye makala ijayo .

0 comments: