Ndugu,
karibu tena katika mwendelezo wa makala ambazo zimekuwa zikitolewa katika blogu
na app ya timiza ndoto ni tumaini langu unaendelea vizuri na kunufaika na
mafunzo haya ambayo kimsingi ukisoma na kuyachukulia hatua ni ngazi pekee ya
kukufanya ufikie malengo yako na kutimiza ndoto zako.
Leo naenda
kuzungumzia swala la msingi sana ambalo linaweza kukufanya ufikie malengo yako
au usifikie malengo yako na kutimiza ndoto zako. NGUVU YA WATU UNAOISHI NAO.
Watu
unaoishi nao ni kipimo tosha cha kukutambulisha kama unaweza kufikia ndoto zako
au la. Kuna msemo wa waswahili ambao unasema
“Ndege wanaofanana huruka pamoja
” kwahiyo kupitia watu unaoishi nao tunapata picha nzima ya maisha yako maana
mawazo na mtazamo mzima wa watu mnaoishi nao ni lazima ufanane. Kama
umezungukwa na watu ambao ni maskini na wana mawazo ya kimaskini hakuna njia
yeyote unayoweza kukwepa umaskini kama utaendelea kuwa nao.
Watu ulioko
nao karibu kama ndugu, jamaa, marafiki na hata wafanyakazi wenza wana ushawishi
mkubwa sana kwako. Unaweza kuwa na mawazo mazuri sana ya kuondoka kwenye
umaskini wako ila unapowapa mawazo yako watu wako wa karibu kama wana mawazo ya
kimaskini watakuwa wa kwanza kukukatisha tamaa. Ni rahisi sana kuwasikiliza kwa
sababu huenda unawaamini sana na pia upo karibu nao sana hivyo unashindwa
kuwapinga. Kwa njia hii unajikuta unaendelea kuwa maskini licha ya jitihada
nyingi unazofanya za kujikwamua kwenye umaskini huo.
Jaribu
kuchunguza vizuri na kwa makini uangalie mfumo wako wa maisha na vitu
unavyofanya havitofautiani sana na vile wanavyofanya watu unaoishi nao kwa muda
mwingi. Wote ni kama mna mfumo mmoja wa maisha utakuta wote mmeajiriwa au
mnafanya biashara , mkitoka kazini labda jioni mnakutana baa kupumzika, hadithi
zenu zinahusisha mambo mengine tofauti tu. Kwa njia hii unajikuta wote mna
uchumi unaofanana. Kama watu unaoishi nao muda mwingi hawana ndoto kubwa kwenye
maisha yao watakuzuia na wewe kuwa na ndoto kubwa. Kama watu hao hawaoni
umuhimu wa kubadili maisha yao, watakuambukiza na wewe tabia hiyo.
Sasa ufanye nini kama umeshagundua
kwamba watu unaoishi nao wanakuzuia kufikia malengo na ndoto zako. Naomba fanya
mambo matatu yafuatayo;
- Punguza muda unaotumia kukaa na watu hao. Jinsi ambavyo unatumia muda mwingi na watu hao ndivyo unazidi kupokea sumu zao. Hivyo kuwa makini na punguza muda unaotumia kukaa na watu hawa , pia angalia ni mambo gani ambayo unaweza kuwashirikisha . kama watu hawa wamekuwa kikwazo kwako kufikia malengo na ndoto zako kwa kukukatisha tamaa acha kuwashirikisha mawazo yako makubwa. Anza kubadili maisha yako taratibu bila ya kuangalia wao wanafanya au kusema nini.
- Anza kutafuta watu ambao wana mawazo makubwa na wenye mafanikio ndo utumie muda mwingi kuwa nao. Kwa kukaa na watu wa aina hii utaanza kuambukizwa tabia zao ambazo zimewafanya wakaendelea. Kwa kusikiliza maongezi yao na kuona mitazamo yao inakuwa rahisi sana kwako kubadili mtazamo wako. Kwa kuwashirikisha watu hawa mipango yako mikubwa watakupa moyo uifanye kwani wengi wao walishapita kwenye hiyo na wanajua inawezekana.
- Kuwa na mshauri mzuri. Mara nyingine ni vizuri kuwa na mshauri ambaye mnakuwa mnakutana kila baada ya muda unamweleza umefikia wapi na changamoto unazokutana nazo na mshauri huyo anakuwa anakufuatilia na kukusaidia jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali unazokutana nazo. Ni vyema mshauri wako awe ni mtu ambaye ameshafanikiwa kwenye hicho unachotaka kufanya. Isiwe unafanya biashara halafu mshauri wako ni mtu ambaye siye mfanyabiashara. Mtu wa aina hii hana msaada mkubwa kwako kwa sababu hajui nadharia ya kile unachokifanya.
Kwa njia yoyote utakayotumia kujiondoa kwenye umasikini hakikisha
umezungukwa na watu ambao wana mawazo kama ya kwako na wanaelekea unakoelekea
kwa kukaa na watu ambao hawana mpango na maisha yao watakunyonya nguvu yote na
mabadiliko yaliyo ndani yako. Ahsante sana kuwa kuwa nami naomba tukutane tena
kwa makala ijayo.UNAFANYA KAZI NA
NANI?


0 comments: