Habari tena
ndugu, ni tumaini langu tena hujambo na unaendelea vizuri. Karibu kwenye
mwendelezo wa makala ambazo nimekuwa nikizitoa katika blogu na app ya Timiza
ndoto. Ndugu kabla sijaendelea kufafanua zaidi kuhusu kichwa tajwa hapo juu
napenda nikusihi kitu kimoja “ Ubora wa mwalimu darasani
unaonekana zaidi pale wanafunzi wake wanapofaulu kwenye mtihani wala siyo
darasani tu namna gani anafundisha”
kwahiyo itakuwa haina maana ya kuendelea kufuatilia blogu na app Timiza
ndoto kama utaishia kusoma tu bila kuchukua hatua sitahiki katika maisha yako.
Naomba twende wote hatua kwa hatua ahsante.
Mpaka sasa
unamfanyia kazi nani? Ni kichwa cha makala chenye swali ambalo linahoji kuhusu
kazi yako. Hebu tafakari.
Unafanya
kazi kukuza mradi wako au unafanya kazi ya kukuza miradi ya watu wengine?
Napenda niseme kitu kimoja cha msingi sana hakika kama unamfanyia mtu mwingine
kazi nafasi ya kutimiza wewe ndoto zako ni ndogo sana. Naamanisha kama mpaka sasa umeajiriwa na huna
mawazo ya kutoka kwenye ajira yako kuna uwezekanao mkubwa sana wa kusikia tu
neon kutimiza ndoto.
Sisemi
kwamba ajira ni mbaya au kwenye ajira huwezi fikia ndoto zako. Hebu tuangalie
hali halisi, kama umeajiriwa angalia sehemu yako ya ajira ni watu gani ambao
wanalipwa fedha nyingi kiasi cha kuwafanya wapate utajiri? Utakuta ni wachache
sana , tena ni wakurugenzi na mameneja wakubwa. Nyie wafanyakazi wengine wa
kawaida mishahara haikutani , yaani mshahara wa mwezi huu unaisha kabla ya
kupata mshahara wa mwezi unaokuja. Hebu tuangalie nafasi ya wewe kufikia
kiwango hicho cha ukurugenzi au umeneja! Ni nafasi ndogo sana kwako wewe kupata
cheo hicho kwa sababu kipo kimoja tu na wenye sifa wanaweza kuwa wengi. Ndio
maana nasema nafasi ya wewe kufikia malengo yako kwa kumfanyia mtu mwingine
kazi yaani kuajiriwa ni ndogo sana.
Kama
umeajiriwa hata ukafanya kazi kwa kiwango kikubwa kiasi gani bado mshahara wako
utakuwa uleule ama utaongezeka kidogo sana. Wakati mwingine unaweza kupewa
pongezi kidogo ambayo hailingani na jitihada zako. Ila kama unafanya kazi yako
mwenyewe iwe umejiajiri au biashara jinsi ambavyo utaongeza jitihada ndivyo
utavyozidi kuongeza kipato chako. Hakuna wa kukupangia kiwango cha kipato ila
wewe mwenyewe.
TUFANYE NINI
KUFIKIA MALENGO YETU?
Kama tayari
upo kwenye ajira anza kufanya mipango ya kujiajiri ama kufungua biashara
baadae. Kama bado hujaingia kwenye ajira weka mipango ya kutoingia kabisa au
panga kuingia kwenye ajira na kukaa muda mfupi tu ili kupata uzoefu na mtandao
na baadae uondoke ukafanye kazi zako. Usisubiri kukaa kwenye ajira mpaka utakapostaafishwa
utashindwa kutimiza malengo yako na ndoto zako.
Ukikaa sana
kwenye ajira unajisahau na unakuwa unawaza matatizo tu unayokutana nayo kwenye
ajira yako na jinsi mshahara ulivyo kidogo na matumizi makubwa. Hebu kwa mara
moja acha kufikiria matatizo hayo ya ajira na ufikiri ni jinsi gani utaondoka
kwenye matatizo hayo. Weka mipango ni lini utaondoka na utakwenda kufanya
nini?.
Tunaishi
kwenye kipindi ambacho tuna fursa nyingi sana za kutengeneza kipato ukiacha
ajira. Angalia ni fursa ipi inayokufaa wewe kisha uanze kujifunza vitu vya
msingi kuhusiana na fursa hiyo. Kikubwa tumia ujuzi ulio nao, tumia uwezo
mkubwa ulio ndani yako pamoja na vipaji vya kipekee ulivyo navyo na angalia
mazingira yanayokuzunguka ili uone ni kitu gani cha tofauti unaweza kufanya.
Kwa
kujiajiri au kufanya biashara unatengeneza uhuru zaidi wa kuweza kupata kipato
kinacholingana na jitihada zako. Pia unaweza kuwasaidia watu wengi zaidi kwa
kutengeneza ajira.
Ni katika
mwendelezo wa makala zinazopatikana katika blogi na app ya Timiza ndoto karibu
tena kwa makala ijayo UMEJITOA?

0 comments: