UTANGULIZI.
Uchumi upo kwenye hali mbaya (Tatters), Kazi yako ipo
hatarini (trouble) na kama una kazi yako hujui ufanye nini?
Ni takribani dunia nzima imekubwa na janga hili la uchumi na
mara nyingi bila hata kupata ufumbuzi wa moja kwa moja lakini pamoja na hayo
yote si swala la kuhoji ni namna gani na kwasababu gani hayo yote yamekuwa
yakitokea ,Swala la msingi ni kwamba ni kwa namna gani tunaweza kuzitumia hizo
taarifa na kuzifanya upande wetu kuwa ni jambo jema la kujivunia na kuweza
kuleta maendeleo upande wetu.
Nimekuwa nikijifunza biashara na kazi mbalimbali kutoka kwa
watu tofauti tofauti , wakiwemo watu mashuhuri walioendelea na ambao
hawajaendelea , wasomi (veryn educated) na ambao hawajasoma lakini kwa namna
moja au nyingine hao wotewamekuwa wakihangaika hangaika na kubaki kulaumu kuwa
uchumi umekuwa ni mgumu sana.
Huwa nafikiria sana kwanini inatokea mtu maskini na mtu
tajiri ingali wanaweza wakawa sehemu moja na wakifanya kazi moja. Kipindi nipo
shule nilisoma sana kwa bidii zote nikitarajia kuwa huru katika maisha haya na
kuamini kuwa Elimu pekee ndio msingi wa Maendeleo lakini kadri nilivyokuwa
nikizidi kusoma mambo yalikuwa tofauti na matarajio yangu. Sikatai kuwa Elimu
siyo msingi wa Maendeleo ila unaitumiaje
Elimu yako katika maendeleo yako.
Nimesoma vitabu mbalimbali vikiongelea juu ya maswala haya
ya uchumi na kupata mwangaza wa kutosha na namna gani tunaweza kupata uzoefu
kuweza kukabiliana na changamoto za uchumi. Na leo napenda nikusihi vitu
vifuatavyo vya msingi katika makala hii ya “Timiza Ndoto”.
1.Tafakari una chagua kutimiza
ndoto zako ili mwisho wa siku uweze kuwa huru kiuchumi wako au kuwa Mtumishi katika maisha yako.
2.Tafakari juu ya
utawala wako wa kifedha ikiwa unaitawala au inakutawala.
Nimekuwa nikijiuliza ni namna gani mtu anawezaje kupata
utajiri (Wealth) na akaweza na kuweza kubakia na utajiri katika maisha yake
yote na asiwe mtumwa tena katika utafutaji na kuweza kustarehe kabisa.
Ndugu kupitia ukurasa huu wa blog ya “Timiza ndoto”
tutajifunza tufanye nini katika karne hii ya 21 ili tuweze kupiga hatua katika
maisha yetu .lakini kabla hatujaanza kuangalia kwa undani ni namna gani
tunaweza kupiga hatua katika maisha yetu napenda nikusihi kitu kimoja cha
msingi sana ambachio katika mihangaiko yako ya kila siku panga kuwa na kazi
yako ambayo inaweza kukuweka huru katika kufanya mambo unayoyataka katika
maisha yako.
Ahsante sana kwa muda wako uliotumia napenda nikukaribishe
katika mwendelezo wa kujifunza ni namna gani tunaweza kupiga hatua katika
maisha yetu.

0 comments: