Imekuwa ni jambo la kawaida kila mwanzo wa kila mwaka watu kuwa na matazamio mbalimbali. Matazamio haya yamekuwa yakilenga hasa afya za watu, staili mbalimbali za maisha ikiwemo kupunguza uzito, kuacha kunywa pombe ,na kuvuta sigara, kupunguza matumizi ya pesa, na hata kufanya uwekezaji.
Lakini pamoja na hayo yote ,wiki chache tu zinapopita
matazamio hayo husaulika hadi mwezi wa kumi na mbili unapokuja tena. Matazamio yamekuwa
ni utangulizi wa kuweka alama kwa mwaka mpya tu. Katika makala hii hebu
tujifunze na kluwa tofauti na ulenge hasa kwenye matazamio yako. Sasa ni namna
gani unaenda kufanya matazamio yako kuwa malengo na klukufanya utimize ndoto
zako.
Zifuatazo ni njia zitakazokufanya na kukusaidia uweze
kufikia malengo yako ili utimize ndoto zako na siyo kubaki na ndoto zisizo
timika.
1.
FANYA MATAZAMIO KUWA NDOTO ZAKO.
Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kuwa na
matazamio na malengo halafu baada ya muda mfupi wanakata tamaa. Malengo
yamekuwa na kufanywa ahadi za kawaida, ambazo zinakaa muda mfupi zinavunjika na
kusahaulika. Ingawa kitendo cha kubadili matazamio hadi kuwa malengo ni kigumu
sana na chenye kuhitaji kutumia akili nyingi hii yote ni kwa sababu Malengo na
Ndoto ni kitu ambacho hupigania ili apate na kuondokana na shida alizonazo. Malengo
ni kitu endelevu ambacho kinahitaji kukisimamia ili uweze kufikia ndoto zako.
2.
YAFANYE MATAZAMIO KUWA RAHISI.
Kosa la kwanza kabisa ambalo watu
bwengi wanalifanya ni kuwa na malengo ambayo yanazidi maisha yao na hii inapelekea kumfanya mtu aweze kukata
tama haraka sana. Mabadiliko siku zote yanachukua muda na kutokana na hili mtu
inakuwa ni vigumu sana kufikia malengo ambayo yanazidi kimo chake.
Kwamfano hauwezi ukawa na
matazamio ya kuwa tajiri mkubwa duniani mwishoni mwa mwaka na wakati kwa sasa
ni panya road. Na mvuta sigara vijiweni badala ya kuwa na mipangoya kuacha kuvuta
sigara uanze mwanzo kama mtoto anayetembea kwa kuwa na matazamio kadri ya uwezo
wako. Malengo yanapokuwa yamesetiwa makubwa kupita kiasi ni rahisi kufeli pindi
mwili na akili zinapochukua muda mrefu kufanya kitu ambacho hakiwezekani .
mabadiliko yanatakiwa kuwa taratibu na siyo harakaharaka.
3.
YAFANYE MATAZAMIO KUWA YA PEKEE.
Wakati unapopangilia mipango yako ya mwaka
, ifanye mipango yako kuwa ya pekee. Upange mipango ambayo itakufanya ufikie
mafanikio yako, mipango inayoainisha ndoto zako. Kama mtazamo wako ni kununua gari sasa unatakiwa uainishe unataka kununua gari
ya aina gani? Rangi yake na uweze kustick kwenye mipango yako ya kununua gari
tu.
Watu mara nyingi huwa wana matazamio kwa
mfanio aweze kupunguza uzito lakini anashindwa kuainisha kuainisha ni uzito wa
kilo ngapi anatakiwa afikie . inakuwa ni vigumu sana kuona mabadiliko kitu
ambachokitamfanya akate tamaa mapema.
4.
AINISHA MIPANGO YAKO.
Unaweza kuchora jedwali kwenye notebook la
namna gani unaweza kufikia na kutimiza malengo yako. Kama malengo yako ni
kutunza shillingi Millioni moja kwa mwaka sasa unatakiwa utengeneze bajeti
ambayo kwa kila mwezi utakuwa unajaza kwenye jedwali lako na ukibainisha
matumizi unayoyafanya. Au kwa mfano mtu ana mpango wa kuingia gym ni muhimu
kubainisha ni gym gani unaenda kufanya, uitafute iko wapi, upange siku na muda
sahihi wa kufanya gym.
5.
FURAHIA KIDOGO ULICHOPATA.
Watu hujifanya wagumu sana wanapokuwa pekee
yao ukilinganisha wakiwa na watu wengine. Wanathubutu kujiadhibu wenyewe na
kusababisha kushindwa kufikia malengo yao, maana unaposhindwa kutambua madogo
uliyonayo utayatambuaje makubwa yale utakayoyapata?
Kusheherekea mafanikio hata kama yakiwa
madogo ni muhimu sana kwa hatua ya mafanikio makubwa.
Kwa mfano unapokuwa na siku yako maalumu
jaribu kuchukua muda hata wa lisaa limoja uweze kujipongeza mwenyewe kwa hatua
uliyofikia hata kama ni ndogo kiasi gani
maana kupitia hicho kitu ulichokipata kitakupa hamasa na kukufanya uzidi kupiga
hatua katika mafanikio yako.
6.
JIAMINI MWENYEWE.
Mwisho ,lakini muhimu sana ni jambo la
kujiamini mwenyewe , hauwezi kufikia malengo yako kama hauamini utayapata. Ni imani yako pekee itakayokufanya
ufikie malengo yako. Inakuwa ni kitu cha ajabu mtu anapopanga kununua gari
halafu hujiamini kama unaweza kununua,. Nguvu zote ambazo tunaanza nazo mwanzoni
mwa mwaka tukijiamini na kwa ujasiri mkubwa hakika tutatimiza ndoto zetu.

0 comments: