Friday, September 28, 2018

TIMIZA NDOTO ZAKO KWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:-




Ndoto imekuwa ni kitendawili ambacho kimekuwa kikikosa jibu la moja kwa moja baina ya watu na kufanya wengi wao wakate tamaa katika safari yao ya kutimiza ndoto zao. Leo napenda kuzungumzia mambo yafuatayo yatakayokusaidia kupiga hatua katika mafanikio yako:-
1.    KUWA IMARA.
Mafanikio yetu yanategemea sana uimara wetu hasa katika upande wa afya zetu,ndugu kama itazolota na kulegea kweli upande wa kufikia malengo yako itakuwa ni kitendawili. Maana afya zetu zinapokuwa imara hapo tunaweza kukumbuka tufanye nini ili kufikia mahala Fulani tunapotaka kufika.
2.    FURAHIA MAISHA YAKO.
Ni kosa la jinai sana inapofikia hatua tunaanza kulaani maisha tuliyonayo , wengi tumekuwa tukilaani sana maisha tuliyonayo kwa sababu ya ugumu wake, changamoto zake n.k. lakini hatukumbuki kupitia hayo maisha tuliyonayo ni fursa pekee ambayo tunaweza kufanya vitu vikubwa ambavyo mwisho wa siku tutafurahia maisha yetu. Ndugu tunapofurahia maisha yetu inatupa chachu na hamasa zaidi katika kufight ndani ya maisha yetu na ndo kitu pekee kitakachomfanya mtu atomize ndoto zake haraka akiwa atafurahia nafasi aliyonayo na kuweza kufanya kazi kwa bidii zote.
3.    FANYA UTALII.
Neno utalii linakuja linatafasiriwa tofauti linapokuja kwenye mindset za watu kuwa hadi usafiri nje ya nchi ndo uwe umefanya utalii. Utalii upo wa aina nyingi ukiwa ni wa  nje au wa ndani na ya nchi. Ndugu unapokuwa unafanya utalii ni nafasi kubwa ya kuweza kujifunza mambo mengi yakiwemo biashara, kilimo, mazingira ya kuishi, uwekezaji n.k. maana unapokuwa unaishi mazingira yaleyale kila kukicha huingizi kitu chochote kichwani, yaani hujaona kitu kipya kwa muda mrefu kuna percentage kubwa sana ya akili kudumaa na kuona kumbe maisha ni hayahaya kwahiyo unapofanya utalii wa mazingira tofauti tofauti unafanya akili yako ifunguke kwa mambo mengi.
4.    TUNZA PESA.
Kati ya vitu ambavyo imekuwa ni mtihani mkubwa mzito ni namna gani ya kutunza pesa? Pesa imetawala kabisa fikira za watu na kushindwa ni namna gani ya kuikabili wanapoipata. Si rahisi sana kutambuia kama pesa inakutawala au laa lakini unapoweza kutunza pesa na kuweza kuifanyia vitu vya msingi ulivyoipangilia kabla hujaipata itakuwa ni rahisi sana kutimiza ndoto zako.
5.    SAIDIA WENGINE.
Kusaidia ni jambo jema ambalo linatakiwa lifanywe kwa kila mmoja wetu. Ndugu tunapokuwa na moyo wa kutoa na kusaidia wengine tunajijengea tabia ya kupokea na sisi na moyo wa utafutaji zaidi maana unapokuwa unatoa unajiandaa kupokea pia.
6.    TAFUTA KAZI MPYA.
Kazi unayofanya isiwe ni kikwazo cha kufikia ndoto zako wengi tumekuwa tukishindwa kuchukua maamuzi yaliyo sahihi hata kama mzigo umetuelemea  katika kazi zetu kwa kuhofia kushindwa kazi nyingine. Pale panapohitaji kuchukuliwa maamuzi yachukuliwe tu maana huwezi jua kilicho mbele yako kabla hujafika huko.


0 comments: