Wednesday, October 3, 2018

LITAMBUE HILI LEO.





Kutokupatikana kwa ajira kunazidi kuongezeka. Je hufikirii kama nyakati zimebadilika. Nani anayejua? Hebu angalia nyuma uone ni jinsi gani ajira zilivyokuwa zinapatikana kwa urahisi halafu angalia na mfumo wa maisha ulivyo sasa hivi ujaribu kulinganisha. Tupo kwenye nguzo ya umeme tumenaswa na hatujui tufanye nini? Akili zetu zimefumbwa na hatuwezi kufanya chochote kama panzi waliotundikwa kwenye mti.
Uchumi sio tatizo.tatizo ni nini? Najua una hasira pengine juu ya mambo ya siasa, rushwa, serikali kutotimiza ahadi zake nzuri, kutokushughulikia haki za msingi za binadamu au labda pengine una hasira wewe kama wewe kutotambua mapema.
Maisha ni magumu sawa lakini swali la msingi unapata wapi suluhisho lake? Lawama na miguno kukaa kujilaumu kwako kila siku hakuwezi kufanya kesho yako iwe vizuri na kama unataka kesho yako iwe vizuri ni lazima uitengeneze leo na njia sahihi ya kufanya ni kuwa na mtazamo chanya katika maisha yako ya baadaye ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira ya kuwa na kazi yako.
Wengi wanajiuliza “sasa ni kazi gani ya kufanya kwenye wakati mgumu huu wa uchumi? “Huu ni wakati mzuri sana katika maana halisi ya neno ujasiriamali kwa maana ya kwamba:,Ujasiriamali unahitaji kutatua changamoto ambazo ni ngumu na wakati mgumu ikiwemo kubuni mbinu ambazo zitafanya mambo yawe rahisi. Unajua wengi wanasema hali ni mbaya kwa sababu wanashindwa kutoa changamoto zao, lakini hebu fikiria ukiwa kwenye shida, changamoto nyingi zimekubali huwa unafanya nini? Pengine huwa unasolve mambo yako bila hata kujua ni njia gani umetumia.
   Watu wengi tumekuwa tukikimbilia ajira serikalini ili mradi tuwe na uhakika wa maisha ya leo. Lakini vipi kuhusu kesho? Uhakika wa kula, kupata pesa hata ukikwama kiafya, majanga mbalimbali yanapotokea kama ajali, vifo na vinginevyo vimekuwa vikitazamwa sana na kusababisha watu kutafuta ajira serikali ili waweze kujilinda na hayo. Na je inapotokea mtu anakoswa kazi anakuwaje? Hakika tumekuwa na mentally disaster ambayo imelaza akili zetu na kushindwa kufikiri ni namna gani tunaweza kuwa na kazi zetu ambazo zinaweza kutuweka financially free.
Simanishi au sisemi kama ajira ni kitu kibaya nayo pia ni njia mojawapo ya kujipatia kipato na kumfanya mtu aweze kuishi vizuri. Maana tafasiri ya neno maendeleo kwenye mind set za watu ni tofauti tofauti lakini tunapokuja kutaka kuwa huru katika uchumi ni lazima tuwe na kazi zetu.


0 comments: