Thursday, March 8, 2018

KIJANA NA HAMASA:UTANGULIZI.



Ndugu, mpendwa ni tumaini langu wewe ni mzima wa afya na buheri tele. Ni jambo la kumshukuru Mungu. Maana ni vitu vingi tunavyokumbana navyo ikiwa ni pamoja na kazi, majukumu, shida, matatizo, huzuni, starehe, misukosuko na mambo mbalimbali kadha wa kadha.
     Imekuwa desturi na jambo la kawaida katika karne hii mtu kuwa na kazi nyingi(busy) na hata kupelekea kukosa muda wa kupumzika na kuperuzi na vitu mbalimbali kwa ajili ya kujitafutia riziki.
      Ikiwa mimi na wewe katika dunia hii ya utandawazi (Globalization) Dunia ambayo imejaa na kuongezeka maarifa ni jukumu letu sote sisi kutafakari ni namna gani tunaweza kuutendea muda wetu sawasawa na dunia inavyokwenda.
      Napenda kutoa shukrani zangu za dhati sana kwa kuchukua na kutoa muda wako kuweza kusoma na kufuatilia ukurasa huu mpya wa “KIJANA NA HAMASA”
Kijana ni nguzo kubwa na muhimu katika familia, ukoo, jamii na hata taifa kwa ujumla. Kijana ni chombo kinachotegemewa sana katika maisha ya mwanadamu ,maendeleo na shughuli zote zinazofanyika.

KWANINI KIJANA NA HAMASA?

     Katika uhalisia Nguzo ni kitu pekee kinachofanya kitu kionekane na hatimaye kiweze kutambulika ni kitu gani? Kijana ni Uti wa Mgongo katika maendeleo na siku zote mafanikio yanakuja pale mtu anapokuwa na hamasa ya maendeleo katika kazi, shughuli anayofanya na kupelekea yeye kujitoa kifikra , mwili hadi kufikia pale anapopahitaji.
KIJANA NA HAMASA Ni ukurasa mpya wa blog unaoelezea na kutoa ushauri mbalimbali ni jinsi gani na namna gani Vijana , Baba , Mama , Mzee unaweza Kujiwezesha na hatimaye Kufikia Malengo na kukamilisha ndoto zako kwa muda sitahiki.
Fuatana name katika ukurasa huu ujue na utambue ni nini unatakiwa kufanya katika karne hii ili uweze kufanikisha ndoto zako ikiwa ni faida kwako , familia yako, ukoo wako , jamii inayokuzunguka na taifa kwa ujumla.
Ahsante sana kwa muda wako naamini utakuwa pamoja nami katika makala zijazo ili tuweze kufanya kile kinachostahili kufanyika ili tuweze kujenga maisha yetu na taifa kwa ujumla.

0 comments: