Magonjwa ya kuku:-
01.UGONJWA WA MDONDO
Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia
kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia asilimia tisini.
Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwa sababu ya usugu mwilini
(body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi.
Ugonjwa huu
husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho Paramyxo viridae na huenezwa kwa
njia ya hewa na kugusana.
DALILI ZAKE.
· -
Kukohoa na kuhema kwa shida.
·
-Ute hutoka mdomoni na puani.
· -
Kuku walioathirika hupata kizunguzungu.
· -
Kuharisha uharo wa kijani na njano.
· -
Kuzubaa, kusinzia na mabawa kushuka.
·
-Baada ya siku 2 kuku hupindisha shingo.
·
-Kuvimba macho.
· -
Kuku hutaga mayai hafifu.
·
-90% ya kuku huweza kufa.
TIBA.
Ugonjwa huu hauna dawa.
KINGA.
Chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu na mara nne kwa
mwaka. Kuna chanjo za aina mbili za ugonjwa huu:-
1.
LASOTA
Chanjo hii hutolewa katika dawa
yenye umbile la kidonge kimoja kimoja ambacho kina dozi ya kuku 1000 na huwekwa
kwenye maji ili kuku wanywe hiyo dawa. Inashauriwa kuku wanaopewa dawa hii
wanyimwe maji ya kunywa siku moja kabla yake.
Ni vizuri kuwapa mchanganyiko
maalumu wa dawa wenye mchanganyiko wa vitamin na dawa ya kuwaongezea kuku
nguvu. Dawa hii itolewe saa moja aui zaidi baada ya kuwapa chanjo ya mdondo.
2 2
THERMOSTABLE I2 NCD VACCINE.
Huwekwa katika chupa kimoja (vial)
chenye dozi 400 za kuku. Chanjo hii inavumilia joto ikikaa bils nje ya jokofu
kwa muda mrefu maana imetengenezwa katika mazingira ya nchi za joto na inaweza
kukaa kwa siku 14-15 ikiwa itatunzwa ipasavyo hata baada ya kutumiwa mara ya
kwanza.
02 KUHARISHA DAMU
(COCCIDIOSIS).
Ugonjwa huu husababishwa na
kimelea cha protozoa cha jamii ya Eimiria (Eimeria,tenela, Eimeria maxima na
Eimeria accervunila).
Kwa kawaida wadudu hawa hupenda kuishi kwenye mazingira
machafu kama vinyesi, vyakula vilivyooza na umaji maji (Moist Environment).
DALILI ZAKE.
· -
Kinyesi chake huchanganyikana na damu.
· -
Wakati mwingine kuku hunya damu.
·
-Kuku hudhoofika sana.
·
-Kuku huteremsha mabawa yake.
·
-Hatimaye vifo hutokea.
TIBA
Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za
i.
Kundi la sulphur:- mfano
sulphonamides (ESB3) kwa siku 3-4.
ii.
Amprolium:- dawa za
ugonjwa huu hupatikana madukani hivyo ukipatwa na tatizo hilo fika kwenye
maduka ya dawa au muone mganga wa mifugo.
KINGA
-Zingatia usafi mara kwa mara kwa kuwa ugonjwa huu huambatana
na maji maji na uchafu wenye vimelea vya ugonjwa huu , ni vizuri kuhakikisha
banda la kuku linakuwa safi na wakati wote
-Tenga kuku wagonjwa kutoka kwa walio wazima na tumia dawa ya kinga ili kuepudha uwezekano
wa kuku kuambukizwa ugonjwa huu. Dawa inayopendekezwa ni zile zinazoitwa (coccidiostat)_ na
tenga kuku wadogo (vifaranga) kutoka kwenye kundi la wakubwa.

0 comments: