Monday, October 8, 2018

MWENDELEZO WA MAGONJWA YA KUKU





03.HOMA YA MATUMBO (FOWL TYPHOID)
Husababishwa na vimelea vya wadudu wa bakiteria wa jamii ya salmonella. Kimelea hicho cha bakiteria huitwa salmonella gallinarum.
DALILI ZAKE
·        - Uharo mweupe au wa kijani.
·         -Vifo hufikia kiasi cha 50%.
·        - Rangi ya minofu hugeuka kuwa ya njano.
·        - Viungo vya ndani kama maini , figo, bandama huvimba.
·        - Maini hung’aa kwenye mwanga mkali.
TIBA
-Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili kutibu ugonjwa huu.
KINGA.
-Chanja kuku wako mara kwa mara. Na fanya usafi wa banda na vyombo vya kulishia na kunyweshea maji ipasavyo.

04 .UGONJWA WA MAFUA YA NDEGE.
Ugonjwa wa mafua ya ndege ni ugonjwa hatari sana kwa kuku na jamii nyingine za ndege na pia ugonjwa huu huwezwa kuambukizwa na kusababisha kifo kwa binadamu. Ugonjwa huu husababishwa na kirusi kiitwacho  ORTHOMYXO VIRUS.
Ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya kugusana baina ya ndege na baina ya ndege na binadamu.
DALILI ZAKE.
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana kwa kipindi cha siku 3-7 baada ya kuku kuambukizwa  na dalili zake hutofautiana kutokana na umri wa ndege. Na baadhi ya dalili ni hizi zifuatazo:-
·       -  Kuku au ndege hupumua kwa shida (dyspnoea).
·       -  Kuzubaa
·       -  Kutokwa na machozi.
·       -  Kukohoa na kupiga chafya.
·       -  Kuharisha kinyesi chenye maji maji.
·         -Sehemu za kichwa zisizo na manyoya huvimba, uvimbe wenye maji maji huonekana kichwani na shingoni.
·       -  Sehemu za juu kichwani hubadilika na kuwa na rangi ya bluu iliyopauka
·        - Kuku hutaga mayai yenye maganda laini.
TIBA
Ugonjwa huu hauna tiba.
KINGA
·         -Toa taarifa kwa mganga (daktari wa mifugo aliye karibu ukiona dalili za ugonjwa huu.)
·         -Tenga mabanda ya kuku wagonjwa na walio wazima.
·        - Fungia kuku wako wasitembee holela.
·        - Acha kununua kuku kutoka eneo linalohisiwa kuwa na ugonjwa huu.
·         -Acha kusafirisha mifugo au ndege bila idhini ya daktari.
·        - Zuia wageni kutembelea mabanda yako ya kuku.
·         -Acha kuhamisha mbolea ya kuku kwenda shambani kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.
·        - Safisha mabanda na kuweka dawa chini ua usimamizi wa mtaalamu wa mifugo na kulipumzisha kwa siku 21 kabla ya kuanza kufuga tena.
·       -  Choma moto mkali au fukia chini mbolea kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa huu.
·        - Pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe
05.GUMBURO (INFECTIONS BURSAL DISEASE);-
Ugonjwa huu husababishwa na kirusi.
DALILI ZAKE.
·        - Hushambulia vifaranga.
·        - Uharo mweupe.
·        - Kuchafuka (dirting of anal area)
·         -Kuvimba
·        - Kiwango kikubwa cha vifo.
·        - Damu hutapakaa eneo la kutolea kinyesi.
KINGA.
·        - Usafi
·       -  Lishe bora
·      -  Chanja vifaranga wakiwa na umri wa wiki tatu kwa kutumia chanjo hai (live vaccine)
06.KIFUA KIKUU CHA NDEGE (AVIAN TUBERCULOSIS- TB)
Husababishwa na kimelea aitwaye mycobacterium avium.
DALILI ZAKE
·         -Kukonda na kupungua uzito.
·        - Vidonda kwenye kishungi.
·         -Kuhara
KINGA
·         -Usafi.
·         -Fanya usafi wa vyombo banda na mazingira.


0 comments: