Tuesday, October 9, 2018

YAFAHAMUE KWA UNDANI ZAIDI MAGONJWA YA KUKU.




MAGONJWA YATOKANAYO NA LISHE (NUTRITIONAL AND METABOLIC DISORDER).
Dalili za magonjwa haya hutegemea aina ya virutubisho vinavyokosekana mwilini kwa mfano ;

  • Kupinda miguu (rickets) husababishwa na upungufu wa vitamin D madini ya calcium na fosiforasi.

  •  Vidonda vyenye damu husababishwa na ukosefu wa vitamin K.

  •  Kichaa cha kuku na kusinyaa kwa misuli husababishwa na upungufu wa vitamin E.

  • Magamba ya mayai (egg shell) kuwa laini ama umbo kuwa bovu husababishwa na upungufu wa madini ya calcium na fosiforasi.

  • Kudonoana husababishwa kwa njia moja au nyingine na upungufu wa chakula na madini ya fosiforasi na calcium.

  •  Kuvimba macho, upungufu wa damu huletwa na upungufu wa vitamin A.

KINGA

  •  Kuwapa kuku mlo kamili.

  •  Kuelewa kwa kina aina za chakula kwa kila rika na aina ya kuku , vifaranga , kuku wa mayai , na wa nyama (Poultry age and classes ie chicks, layers and boilers.)
  •  Kufanya uchunguzi wa virutubisho vilivyomo katika aina ya chakula unachotumia.
MINYOO (HELMINTHIASIS).
Minyoo iko aina tatu kama vile minyoo kamba , minyoo bapa , na minyoo ya mviringo.
DALILI ZAKE
  • Kudumaa
  • Kuwa na manyoya hafifu.
  •  Kupunguza uzito.
  •  Kukonda.
  •  Minyoo huonekana kwenye kinyesi.
KINGA
  • Fanya usafi wa banda vyombo , na mazingira.
  • Tenga vifaranga kutoka kwa wale wakubwa.
  • Badilisha matandazo kuondoa mazalia ya minyoo.
  • Badilisha matandazo kila baada ya miezi mitatu.
TIBA.
Tumia dawa zinazopendekezwa na wataalamu hasa zile zinazoua minyoo ya aina yote mfano piperazine citrate. Na hakikisha kila baada ya miezi mitatu unawapa kuku wako dawa za minyoo.

KUPE , UTITIRI , CHAWA , NA VIROBOTO.
Kupe laini waitwao argus persicus , chawa na viroboto wanaong’ata.
DALILI ZAKE
  • Kujikung’uta
  • Kupiga kelele.
  •  Kiasi cha damu hupungua mwilini.
  •   Utando wa ngozi ndani ya kope za macho hupauka.
  •  Utando wa ngozi juu ya mwili huwa mnene.
  •  Magamba ya unga unga hudondoka.
KINGA.
Tupa au choma masalia ya mayai yasiyoanguliwa na magamba ya mayai yaliyoanguliwa vifaranga na safisha banda mara kwa mara na kunyunyuzia dawa zinazopendekezwa na wataalamu za kunyunyuzia kwenye banda la kuku mfano sevin , akheri powder n.k (dawa hizi ni unga).

0 comments: