Tuesday, October 9, 2018

VITU WANAVYOFIKIRIA VIJANA WA LEO



Tupo kwenye ulimwengu wa utandawazi, uliojaa maarifa ya kila aina , ulimwengu ambao upo kwenye stage ya information age. Ni wazi kuwa mambo yamerahisishwa kila sekta, watu tunaishi kama tupo kwenye kijiji kimoja. Mtu anapata mawasiliano na mtu aliye mbali kwa muda mfupi tofauti na kipindi cha nyuma kitu ambacho kilikuwa kinagharimu muda mrefu.
Kuna faida nyingi sana za utandawazi tulio nao tukiutumia vizuri. Lakini naomba tukumbuke penye faida , hasara hazikosekani. Hebu tuangalie ni nini hasa vijana wa leo tumeathiriwa na utandawazi huu ambao kwa upande mwingine umetufanya kuwa watumwa.
1.  Kila kitu kinawezekana (Everything is possible).


Ni kweli kila kitu kinawezekana endapo tu jitihada binafsi zitatumika lakini imekuwa ni viceversa kwa vijana wa sasa maana urithi mkubwa wa mafanikio yao (muda) wanautumia vibaya na kuwa na logic za tofauti na mafanikio yao lakini hawajui kwamba ‘’Thinking success without struggling is as cooking an empty pot and waiting for soup.’’ 

2. Kutimiza ndoto ni kama kulala na kuamka.



Maendeleo ni mabadiliko kutoka sehemu ya chini hadi juu (gradual changes from low level to high level)  kwa maana ya mabadiliko ni kitu kinachochukua muda kwa maana ni kitu endelevu siyo kitu cha kulala na kuamka. Sasa inapofikia stage hii vijana tulio wengi tunachanganyikiwa na kuanza kuamini imani za tofauti ikiwemo kuamini utajiri kutoka nguvu za ngiza hasa (free mason). Na kushindwa kuchukua maamuzi yaliyo sahihi katika kufikia ndoto zetu.

3. Muda ni kitu cha kawaida tu.


Hakika katika vitu ambavyo hasa vijana hatujali ni muda yaani tunaona kama swala la kawaida tu ambalo hata kesho tutakuwa hivyo hivyo. Lakini napenda nikuambie mafanikio yangu na yako yanategemea sana muda tulio nao na tusije tukafikiri muda huu tunaouchezea utakuja kujirudia tena

1 comment:

  1. Its a nice app but there is no new updates,,,last posts ending 10 months ago,,how can we get new

    ReplyDelete